1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSri Lanka

Raia wa Sri Lanka wapiga kura ya kumchagua rais

21 Septemba 2024

Zoezi la upigaji wa kura katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Urais nchini Sri Lanka tangu mzozo mkubwa wa kiuchumi nchini humo limekamilika Jumamosi huku maafisa wakisifu wapiga kura kwa wingi wao.

https://p.dw.com/p/4kvnn
Sri Lanka I Colombo | Uchaguzi wa rais
Raia wa Sri Lanka wamekamilisha zoezi la kupiga kura ya kumchagua rais wa nchi yao Jumamosi.Picha: Ishara S. Kodikara/AFP/Getty Images

Zoezi la upigaji wa kura katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Urais nchini Sri Lanka tangu mzozo mkubwa wa kiuchumi nchini humo limekamilika Jumamosi huku maafisa wakiripoti idadi kubwa ya watu waliojitokeza kushiriki zoezi hilo.

Maafisa wa uchaguzi wamesema hakukuwa na matukio makubwa ya kuhatarisha uchaguzi huo kote nchini humo. Zaidi ya maafisa wa polisi 60,000 wakiungwa mkono na vikosi vya usalama walisambazwa kote Sri Lanka kusimamia uchaguzi huo huku maafisa 250,000 wakisaidia katika kufanikisha mchakato huo wa uchaguzi.

Soma zaidi. Raia wa Sri Lanka wanapiga kura kumchagua rais leo

Zaidi ya watu milioni 17 walikuwa na sifa za kupiga kura katika vituo 13,421 nchini tangu saa moja asubuhi hadi saa kumi jioni kwa saa za Sri Lanka.

Itakumbukwa kuwa huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu maandamano makubwa yaliyochochewa na mgogoro wa kiuchumi na yaliomuondoa madarakani Rais Gotabaya Rajapaksa mnamo mwaka 2022.