SiasaMali
Raia wa Mali wakabiliana na maisha magumu tangu mapinduzi
19 Agosti 2024Matangazo
Raia hao wamesema tangu mapinduzi ya mwaka 2020, kunashudiwa ongezeko la matatizo ya kiusalama, kiuchumi na pia tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara jambo linaloathiri shughuli za biashara.
Tathmini ya Benki ya Dunia imeonyesha kuwa ukuaji wa uchumi wa Mali unatarajiwa kupungua hadi asilimia 3.1 mwaka huu kutoka asilimia 3.5 mwaka jana, huku viwango vya juu vya umaskini vikiongezeka.
Takriban asilimi 90 ya wakazi wa Mali wanaishi katika umaskini.