1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Raia wa Malaysia wapiga kura kuchaguwa wabunge

12 Agosti 2023

Raia nchini Malaysia wanashuka vituoni kwenye majimbo sita kuchaguwa wabunge wao katika uchaguzi unaotazamwa kama kipimo cha uungwaji mkono wa serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Waziri Mkuu Anwar Ibrahim.

https://p.dw.com/p/4V5Z3
Anwar Ibrahim
Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar IbrahimPicha: Mohd Firdaus/NurPhoto/picture alliance

Ingawa uchaguzi wenyewe huenda usiwe na athari ya mara moja kwa wingi wake wa viti bungeni, lakini wachambuzi wanasema uwezo wake wa kuongoza utakuwa mashakani endapo muungano wa vyama anaouongoza, Pakatan Harapan, utapoteza uungwaji mkono, hasa miongoni mwa jamii ya Waislamu wa Malay, walio wengi zaidi katika taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia. Vituo vilifunguliwa saa mbili asubuhi ya leo kwa majira ya Malaysia, ambapo takribani wapigakura milioni 10 walitazamiwa kuchaguwa wabunge 245 kwenye majimbo ya Kelantan, Teregganu, Kedah, Penang, Selangor na Negeri Sembilan. Miongoni mwa majimbo hayo sita, muungano wa Anwar unashikilia matatu na yaliyosalia yako mikononi mwa chama kinachoungwa mkono zaidi vijijini, kinachoongozwa na waziri mkuu wa zamani, Muhyiddin Yasssin.