1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Guinea afariki kituo cha wahamiaji Mülheim

Josephat Charo
7 Januari 2024

Mhamiaji mwanamume raia wa Guinea amekufa katika kituo cha wahamiaji mjini Mülheim baada ya kukabiliana na polisi

https://p.dw.com/p/4ax76
Deutschland Mülheim an der Ruhr | Toter nach Polizeieinsatz an Flüchtlingsunterkunft
Gari ya polisi nje ya kituo cha wahamiaji mjini Mülheim ambako mwanamume wa Guinea alifariki kufuatia operesheni ya polisi.Picha: Justin Brosch/dpa/picture alliance

Mwanamume wa umri wa miaka 26 raia wa Guinea amekufa baada ya kukabiliana na maafisa wa polisi katika kituo cha kuwapokea wahamiaji katika mji wa Mülheim magharibi ya Ujerumani. Polisi wameitwa katika kituo hicho na wakala wa usalama uliosema mwanamume huyo alikuwa amewashambulia maafisa wake. Wakati polisi walipowasili mwanamume huyo alikuwa chumbani kwake na akawashambulia.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi walijaribu mara mbili kumdhibiti wakati walipomkimbiza katika kituo hicho. Baadaye walifanikiwa baada ya maafisa wawili kuumwa na afisa mwanamke kupigwa kichwani. Magari ya kubebea wagonjwa yaliitwa kusaidia wakaazi na maafisa hao wawili. Mhamiaji huyo wa Guinea alipoteza fahamu alipokuwa akitibiwa ndani ya gari la wagonjwa na baadaye kupelekwa hospitali ambako alifariki dinia.

Polisi katika mji jirani wa Bochum wanafanya uchunguzi wa mauaji kama utaratibu wa kawaida wakisubiri ripoti ya uchunguzi wa daktari. Maafisa waliohusika katika tukio hilo wanapewa ushauri nasaha.