1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Belarus wamshtaki Lukashenko Ujerumani

5 Mei 2021

Kundi la raia wa Belarus limefungua kesi ya uhalifu nchini Ujerumani dhidi ya rais Alexander Lukanshenko na wafuasi wa chama chake kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

https://p.dw.com/p/3szth
Khatyn Jahrestag des Massakers in Belarus
Picha: Viktor Tolochko/Sputnik/dpa/picture alliance

Mawakili wanawawakilisha wahanga wa mateso wamewasilisha madai dhidi ya Lukashenko na maafisa wengine wa usalama kwenye ofisi ya mashitaka ya shírikisho katika mji wa Karsruhe.

Ofisi hiyo imelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba imepokea madai hayo.

Mawakili hao wamesema wamethibitisha mifano zaidi ya 100 ya machafuko, mateso ya kupanga na ukandamizaji mwingine, kufuatia hatua kali zilizochukuliwa na serikali dhidi ya waandamanaji kwa madai ya udanganyifu kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.

Lukashenko alishinda muhula wa sita katika uchaguzi wa Agosti, uliokosolewa kimataifa na upinzani kwa udanganyifu.