1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Raia 6 wa kigeni mbaroni kwa kutaka kumuua Rais wa Venezuela

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Raia sita wa kigeni wamekamatwa Venezuela kwa tuhuma za kupanga njama za kutaka kumuuwa Rais Nicolas Maduro. Miongoni mwao ni raia watatu wa Marekani, wawili wa Uhispania na mtu mwingine mmoja wa Jamhuri ya Czech.

https://p.dw.com/p/4kdg7
Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas MaduroPicha: Ariana Cubillos/AP/picture alliance

Kupitia televisheni ya taifa, Waziri wa mambo ya ndani  wa Venezuela Diosdado Cabello alidai kuwa raia hao wa kigeni walikuwa sehemu ya mpango wa Shirika la Ujasusi la Marekani la CIA la kuipindua serikali ya Venezuela na kuwauwa viongozi kadhaa.

Soma zaidi: UN yaelezea wasiwasi kuhusu mazingira ya hofu Venezuela

Miongoni mwa raia wa tatu wa Marekani waliokamatwa ni pamoja na Afisa wa jeshi la wanamaji Wilbert Joseph Castañeda Gomez. Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ilithibitisha kukamatwa kwa mwanajeshi huyo lakini iliongeza kuwa madai yoyote ya nchi hiyo kuhusika kupanga kumpindua Maduro ni ya uongo.