1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Upigaji kura wa mapema waanza nchini Afrika Kusini

27 Mei 2024

Upigaji kura wa mapema umeanza leo nchini Afrika Kusini katika uchaguzi mkuu, huku wale watakaokuwa makazini na walio na mahitaji maalum, wakipewa nafasi ya kupiga kura zao.

https://p.dw.com/p/4gLUF
Afrika Kusini | Uchagzi 2024
Mabango ya wagombea mbalimbali kwenye uchaguzi ulioanza kufanyika nchini Afrika KusiniPicha: Themba Hadebe/AP Photo/picture alliance

Kulingana na Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, karibu watu milioni 1.6 kati ya milioni 27.6 waliojiandikisha kupiga kura, wamepewa fursa ya kupiga kura zao mapema.

Mawakala wa uchaguzi watawatembelea majumbani kwao zaidi ya watu laki sita walio na changamoto za kutembea. Hapo Jumatano, taifa zima la Afrika Kusini ndipo litakaposhiriki zoezi hilo la upigaji kura, miongo mitatu baada ya kuanza kwa demokrasia nchini humo mwaka 1994.

Kura hiyo huenda ikawa ya kihistoria kama inavyooneshwa na tafiti za maoni zinazotabiri chama tawala cha African National Congress ANC huenda kikapoteza wingi wake bungeni kwa mara ya kwanza.