Qatar yaendeleza juhudi za kuachiliwa mateka wa Israel
15 Novemba 2023Qatar imezitolea wito pande zinazohusika katika mzozo wa Gaza, Israel na Hamas kufikia makubaliano ya kuwaachia mateka, ikionya kwamba hali inayoendelea Gaza inazidi kuwa mbaya kila kukicha.
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Qatar, Majed bin Mohammed Al-Ansari amesema hali inayozidi kuzorota katika Ukanda wa Gaza inatatiza juhudi za upatanishi.Duru zaarifu juu ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kwa muda Ukanda wa Gaza
Taifa hilo limeongoza juhudi za mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas na usitishaji mapigano kwa muda sasa.
Itakumbukwa kwamba siku ya Jumatatu, kundi la Hamas lilidai kuwa, Israel imeomba kuachiliwa huru kwa wanawake na watoto wapatao 100 kwa mabadilishano ya watoto 200 wa Kipalestina na wanawake wanaoshikiliwa katika jela za Israel.