Qatar kuongeza uzalishaji wa gesi asilia ya kimiminika
25 Februari 2024Qatar itaongeza uzalishaji wa gesi licha ya kushuka kwa kasi kwa bei ya gesi duniani, ikisonga mbele na mipango ya kuchimba zaidi rasilimali hiyo huku kukiwa na ushindani mkali na wapinzani kama vile Marekani.
Mkuu wa shirika la nishati la Qatar, Saad al-Kaabi ametangaza hii leo juu ya upanuzi mpya wa uzalishaji wa gesi asilia ya kimiminika ambao utaongeza tani milioni 16 kwa mwaka.
Soma: Umoja wa Falme za Kiarabu wakubali kusambaza gesi na dizeli nchini Ujerumani
Tangazo la Qatar linatolewa wakati bei ya biashara ya gesi ya Marekani ikiporomoka baada ya muongo mmoja wa kupanda kwa uzalishaji ambao uliifanya Washington kuwa miongoni mwa wauzaji wa juu wa mafuta na gesi nje ya nchi.
Bei ya gesi barani Ulaya pia iliporomoka kwa kasi baada ya kushuka kwa usambazaji wa Urusi licha ya Marekani na Qatar kusaidia kuzipa pengo la kiasi kilichopotea.