Qatar inatathmini jukumu lake la upatanishi Israel na Hamas
18 Aprili 2024Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Mohammed bin Abdulrahman bila kutaja yeyote,amewaambia waandishi wa habari kwamba jukumu la Qatar limetumiwa vibaya na baadhi ya watu kutokana na ukomo wa maslahi ya kisiasa.
Aidha ameongeza kwamba hatua hiyo imeisababisha Qatar kufanya tathmini kamili juu ya jukumu lake lililofungamana na mukhtadha wa kibinaadamu. Hapo awali bin Abdulrahman alisema mazungumzo kati ya Israel na Hamas ya kutafuta makubaliano ya usitishwaji mapigano katika Ukanda wa Gaza yamekwama.
Soma pia:Kiongozi wa Hamas asema hakuna mabadiliko katika mazungumzo ya Cairo
Qatar, Marekani na Misri wamekuwa wakisimamia mazungumzo ya wiki kadhaa ambayo pia yangeliwezesha kuachiliwa kwa mateka wa Israel pamoja na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel.