SiasaKorea Kaskazini
Pyongyang yaonya kuhusu ushushushu wa washirika wa Marekani
13 Mei 2024Matangazo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini, leo Jumatatu, imelaumu uingiliaji kati kijeshi katika kanda hiyo, kwa kisingizio cha kufuatilia ukiukaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Korea ya Kaskazini imezitaka Ujerumani, Ufaransa,Uingereza, Australia, New Zealand na Canada, kuacha mara moja uchochezi unaosababisha mvutano na ukosefu wa utulivu.
Korea Kaskazini imesisitiza kuwa itachukua hatua zinazohitajika kutetea mamlaka na usalama wa nchi yake.
Mvutano kwenye eneo hilo ni mkubwa. Mnamo mwezi uliopita, Marekani ilifanya luteka za kijeshi za siku mbili katika eneo la Asia-Pasifiki, zilizowahusisha wanajeshi wa Korea Kusini na Japan.