SiasaKorea Kaskazini
Matamshi ya Blinken kuhusu Pyongyang na Urusi yakosolewa
11 Novemba 2023Matangazo
Blinken alitoa matamshi hayo alipokuwa ziarani nchini Korea Kusini mapema wiki hii ambapo alisema ushirikiano wa kijeshi kati ya Moscow na Korea Kaskazini "unaimarika na kuwa hatari" na akairaia China, iliyo mshirika wa karibu wa Pyongyang kutumia ushawishi wake kuidhibiti dola hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Korea Kaskazini imesema matamshi hayo yanazidisha hali ya wasiwasi kwenye rasi ya Korea na kanda nzima na kuitaka Washington "ijifunze kuzoea uhalisia mpya wa uhusiano kati ya Urusi na Korea Kaskazini".
Mataifa ya magharibi na washirika wake yanatiwa mashaka na kujongeleana kwa nchi hizo mbili zilizo chini ya vikwazo vya kimataifa na zenye uwezo mkubwa wa kijeshi.