SiasaKazakhstan
Putin na Xi watazamia kuongeza ushawishi wao mkutano wa SCO
3 Julai 2024Matangazo
Rais wa urusi Vladimir Putin amewasili katika Mji Mkuu wa Kazakhstan, Astana, asubuhi ya leo kwa mkutano wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai SCO, ambalo ni kundi linaloongozwa na China na kuyajumuisha mataifa ya Asia ya Kati, India na Iran.
Soma pia: Japan, Korea Kusini zatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi
Kiongozi wa China Xi Jinping aliwasili huko Kazakhstan hapo jana na viongozi hao wawili wanalitazama shirika hilo la SCO kama chombo muhimu cha kuendeleza malengo yao ya kimkakati katika kanda ya Ulaya na Asia.
Urusi na China wamezidisha uhusiano wao wa kisiasa, kijeshi na kiuchumi tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake Ukraine.