1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin kukutana na Erdogan leo kujadili makubaliano ya nafaka

4 Septemba 2023

Rais wa Urusi Vladmir Putin na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wanakutana leo mjini Sochi nchini Urusi ambapo wanatarajiwa kuvutana kuhusu suala la makubaliano muhimu ya nafaka.

https://p.dw.com/p/4VvAY
Erdogan und Putin (Archivbild)
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na mwenzake wa uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Sputnik/Xinhua/IMAGO

Taarifa zinasema tayari droni za Urusi zimeshambulia bandari kubwa ya Ukraine ya usafirishaji nafaka,na kuharibu maghala na majengo kadhaa saa chache kabla ya mkutano wa viongozi hao.

Urusi ilikataa kuyarefusha makubaliano hayo mnamo mwezi Julai ikilalamika kwamba usafirishaji wa nafaka na mbolea yake unatatizwa kutokana na vikwazo vinavyohusiana na vita nchini Ukraine,vilivyowekwa na nchi za Magharibi zinazoiunga mkono Ukraine. 

Soma pia:Mkataba wa Bahari Nyeusi: Umoja wa Mataifa watuma pendekezo jipya kwa Urusi

Makubaliano hayo ya Nafaka kati ya Uturuki na Urusi ndiyo yaliyofungua njia ya usafirishwaji salamawa nafaka kutoka Ukraine, kupitia bahari nyeusi kipindi cha mapigano na kupunguza adha ya ukosefu wa  nafaka duniani.

Uturuki inaitaka Urusi iondowe vizuizi ilivyoweka lakini rais Putin ameshikilia kwamba makubaliano hayo hayatorefushwa hadi masharti kadhaa ya Urusi, yatakapozingatiwa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW