1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin kutohudhuria mkutano wa kilele wa BRICS, Afrika Kusini

19 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladmir Putin hatahudhuria mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi uliwenguni - BRICS nchini Afrika Kusini mwezi ujao kwa tishio la kukamatwa.

https://p.dw.com/p/4U8BT
Russland I Vladimir Putin
Picha: Alexander Kazakov/Kremlin Pool/IMAGO

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imeyasema hayo, na kuhitimisha miezi mingi ya uvumi kuwa angekamatwa. Ziara hiyo ya Putin lilikuwa suala tete la kidiplomasia kwa serikali ya Afrika Kusini.  Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa, Vincent Magwenya, amesema kufuatia makubaliano ya pande mbili, Rais wa Urusi Vladmir Putin hatohudhuria mkutano huo wa kilele. Badala yake, Waziri wa Mambo ya Kigeni Sergei Lavrov ataiwakilisha Urusi. Amesema uamuzi huo unafuatia mashauriano kadhaa yaliyofanywa na Ramaphosa katika miezi ya karibuni, na ya karibuni kabisa yakiwa jana usiku.

Putin analengwa na waranti ya kukamtwa ya mahakama ya ICC

Kiongozi huyo analengwa na waranti wa kukamatwa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai - ICC, kifungu ambacho Afrika Kusini kama mwanachama wa ICC anatarajiwa kukitekeleza kama Putin angezuru nchini humo. Afrika Kusini ni mwenyekiti wa sasa wa kundi la BRICS, linaloyajumuisha madola ya Brazil, Urusi, India na China.