SiasaUrusi
Putin awasili Astana kushiriki mkutano wa Shanghai
3 Julai 2024Matangazo
Putin anatazamiwa kukutana na rais wa China Xi Jinping na Tayyip Erdogan wa Uturuki.
Mara ya mwisho, Putin kukutana na Rais Xi ilikuwa mwezi Mei, wakati alipoitembelea China katika ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi baada ya kuapishwa kwa muhula wa tano kama rais wa Urusi.
Soma pia:Putin kusaini mikataba ya ushirikiano wakati wa ziara mjini Pyongyang
Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO ni jukwaa la kimataifa la kisiasa, kiuchumi, na kiusalama lililoanzishwa na China na Urusi mwaka 2001. Linajumuisha nchi wanachama ambao ni India, Iran, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Pakistan, Tajikistan na Uzbekistan.
Uturuki, ambayo si mwanachama wa jumuiya hiyo, mara nyingi imekuwa ikishiriki katika mikutano yake kama mbia wa mazungumzo.