1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Putin asema vita vya Ukraine vinachukua mkondo wa kidunia

22 Novemba 2024

Rais Vladimir Putin amesema vita vya Ukraine vinageuka kuwa mgogoro wa kidunia. Hii ni baada ya Marekani na Uingereza kuiruhusu Ukraine kuishambulia Urusi na silaha inazopewa na nchi hizo.

https://p.dw.com/p/4nIRg
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Putin amezionya nchi za Magharibi kuwa Moscow inaweza kujibu mashambuliziPicha: Vyacheslav Prokofyev/Sputnik/Kreml Pool/AP/picture alliance

Putin amezionya nchi za Magharibi kuwa Moscow inaweza kujibu mashambulizi hayo. Ametangaza kuwa Urusi imetumia aina mpya ya kombora la masafa ya kati, kushambulia kituo cha kijeshi cha Ukraine. Putin amesema, baada ya idhini kutoka kwa serikali ya Joe Biden, Ukraine iliipiga Urusi na makombora sita yaliyotengenezwa na Marekani aina ya ATACMS mnamo Novemba 19 na makombora ya Uingereza ya Storm Shadow Novemba 21.

Soma pia: Zelensky adai Putin aigeuza Ukraine uwanja wa majaribio ya silaha zake

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa viongozi wa dunia kujibu vikali matumizi ya Urusi ya kombora jipya la masafa marefu. Amesema hatua hiyo ya Urusi inaongeza kiwango cha ukatili katika vita vyake dhidi ya Ukraine. Zelensky amesema huo ni ushahidi wa mwisho kuwa Urusi bila shaka haitaki amani.