Migogoro
Putin asema Ukraine itapokea jibu stahiki uvamizi Kursk
13 Agosti 2024Matangazo
Kyiv ilifanya shambulio la kustukiza ndani ya mkoa wa magharibi mwa Urusi wa Kursk Jumanne jioni, na kuteka maeneo zaidi ya 25, katika shambulio kubwa zaidi kwenye ardhi ya Urusi tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Mkuu wa majeshi ya Ukraine Oleksander Syrsky alimuambia Rais Volodymyr Zelenskiy katika vidio iliyochapishwa Jumatatu, kuwa vikosi vyake vinadhibiti karibu kilomita za mraba 1,000 za ardhi ya Urusi na vinaendeleza mashambulizi.
Putinameuambia mkutano wa maafisa wa serikali kwamba moja ya malengo ya wazi ya adui ni kuchochea mfarakano na kuharibu umoja na mshikamano wa jamii ya Urusi, na kuonya kuwa Ukraine itapokea jibu linalostahili.