Putin aahidi majibu ya mashambulizi ya Ukraine kuwa mabaya
10 Oktoba 2022Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema jibu la Urusi katika mashambulizi zaidi nchini Ukraine litakuwa ni baya zaidi baada ya vikosi vya Mocsow kufanya mashambulizi ya kulipa kisasi kote Ukraine. Katika hotuba yake ya televisheni Putin amesema ilikuwa ni kitu kisichowezekana kuacha kujibu mashambulizi ya Ukraine. Ameongeza ikiwa mashambulizi aliyoyaita ya kigaidi yataendelea, basi majibu ya Urusi yatakuwa mabaya zaidi
"Ikiwa majaribio ya kufanya mashambulizi ya kigaidi katika eneo letu yataendelea, majibu ya Urusi yatakuwa mabaya na yanalingana na kiwango cha vitisho vinavyotolewa dhidi ya Shirikisho la Urusi. Hakuna mtu anayepaswa kuwa na shaka juu ya hili."
Katika hatua nyingine Rais huyo wa Urusi anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Uturiki Recep Tayyip Erdogan baadae wiki hii kujadili pendekezo la Uturuki kusimamia mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema Urusi haijapokea ishara yoyote kuhusu mazungumzo hayo lakini haiondoi nia ya Putin kujadili na Erdogan.