Putin aamuru jeshi kuwang'oa mpakani askari wa Ukraine
12 Agosti 2024katika kile kinachotajwa kuwa operesheni kubwa ya kuvuka mpaka iliyofanywa na Ukraine tangu Moscow ilipoivamia nchi hiyo miaka miwili iliyopita.
Putin ametoa matamshi hayo alipozungumza na maafisa wa serikali yake kuhusiana na kisa hicho ambacho hadi sasa kimelazimisha mamia kwa maelfu ya Warusi kuhamishwa kutoka kwenye mkoa wa mpaka wa Kursk.
Zaidi kuhusu wajibu wa vyombo vya usalama vya Urusi, Putin amesema: "Jukumu la msingi la Wizara ya Ulinzi ni kumtimua adui ndani ya ardhi yetu na kwa pamoja na walinzi wa mipaka kutoa ulinzi madhubuti wa mipaka. Bila shaka adui atapata jibu la uhakika na malengo yetu yote yatatimizwa".
Soma pia: Jeshi la Urusi lakiri mafanikio ya Ukraine katika mashambulizi ya Kursk
Ukraine ilianzisha operesheni hiyo ya kustukiza jumanne iliyopita kwa kuwatuma wanajeshi wake kuvuka wa Urusi kupitia mkoa wa Kursk na kufanikiwa kukamata maeneo kadhaa ya makaazi. Watu 12 wameuwawa na wengine 120 wamejeruhiwa kutokana na uvamizi huo.