1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA:Makamu wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma kushtakiwa

20 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF1c

Msemaji wa Uendeshaji mashataka wa serikali nchini Afrika Kusini amesema makamu wa rais wa zamani nchini humo Jacob Zuma atashtakiwa kwa madai ya rushwa.

Makhosini Nkosi amesema mashataka yatakayomkabili bwana Zuma ni pamoja na visa viwili vya ulaji rushwa.

Rais Thabo mbeki alimfukuza kazi Zuma baada ya mahakama kumpata na hatia mfanyibiashara Schabir Shaik ya makosa ya Rushwa na udanganyifu.

Waendesha mashtaka wanasema wana uhakika wa kushinda kesi hiyo dhidi ya Zuma.

Hata hivyo uchunguzi wa mwanzo juu ya madai ya Rushwa kwa bwana Zuma ya mwaka 2003, waendesha mashtaka walikosa ushahidi wa kutosha dhidi ya makamu huyo wa zamani war ais.

Bwana Zuma ameshikilia kusema hana hatia na kwamba madai hayo ni njama zilizonuiwa kummaliza kisiasa.

Nchini Afrika Kusini iwapo mtu anapatikana na hatia ya rushwa anakumbana na kifungo cha miaka 15 jela.