1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Polisi ya Uturuki yawatia mbaroni waandamanaji 200

2 Mei 2024

Polisi wa Uturuki jana Jumatano walifyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira pamoja na kuwaweka kizuizini zaidi ya waandamanaji 200.

https://p.dw.com/p/4fP9O
Machafuko ya Istanbul katika Siku ya Wafanyakazi
Maafisa wa polisi wa Uturuki wakikabiliana na waandamanaji wanaojaribu kuandamana kuelekea uweanja wa Taksi.Picha: KEMAL ASLAN/AFP

Polisi wa Uturuki jana Jumatano walifyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira pamoja na kuwaweka kizuizini  zaidi ya waandamanaji 200 baada ya mamlaka kupiga marufuku mikusanyiko ya kuadhimisha ya Mei Mosi iliyopangwa kufanyika katika uwanja wa kihistoria wa taifa hilo wa Taksim huko mjini Istanbul.

Waandishi wa AFP wameripoti kuwa polisi walikabiliana na waandamanaji karibu na ukumbi wa jiji katika wilaya ya Sarachane, wakifyatua mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwazuia waandamanaji kuvunja vizuizi.

Waziri wa mambo ya ndani Ali Yerlikaya aliandika kwenye ukurasa wake wa X, zamani Twitter kwamba, watu 210 wamekamatwa Istanbul kwa kutotiii onyo lao na kuwashambulia polisi siku ya Mei Mosi.

Zaidi ya polisi 40,000 walisambazwa kote Istanbul, wakizuia hata mitaa midogo ya pembeni kwa vizuizi vya chuma katika jaribio la kuzuia waandamanaji kukusanyika.