1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Polisi ya Korea Kusini yaombwa kumkamata rais Yoon

6 Januari 2025

Polisi wa Korea Kusini wametakiwa kumkamata rais aliyesimamishwa kazi Yoon Suk Yeol, shirika la habari nchini humo la Yonhap limeripoti mapema leo Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4oqrk
Südkorea | Präsident Yoon Suk Yeols Ansprache in seinem Amtssitz in Seoul
Rais aliyewekwa kando Korea Kusini, Yoon Suk Yeol akitoa hotuba ya hadhara kutoka katika makazi yake rasmi mjini Seoul.Picha: South Korean Presidential Office/Handout/Yonhap/AFP

Timu ya wachunguzi wanaofanya kazi ya Upelelezi wa Rushwa kwa Viongozi wa Vyeo vya Juu (CIO) ilijaribu kutekeleza hati ya mahakama ya kumkamata Yoon siku ya Ijumaa baada ya kiongozi huyo kupuuza mara tatu wito wa kwenda kuhojiwa kutokana na jaribio lake la kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi mnamoDesembatatu mwaka uliopita. Polisi nchini humo sasa wameombwa kutekeleza kibali hicho ingawa hata hivyo bado wataamua ikiwa watashirikiana na timu ya wachunguzi inayofanya upelelezi au la. Hapo jana, maelfu ya raia wa Korea Kusini waliandamana nje ya makazi ya Yoon mjini Seoul. Kambi moja ikitaka Yoon akamatwe huku nyingine ikitaka kushtakiwa kwake kutangazwe kuwa ni batili.