Polisi Ujerumani wafanya msako wa walanguzi wa binadamu
24 Septemba 2024Polisi nchini Ujerumani imefanya msako katika majengo kadhaa kusini magharibi mwa nchi hiyo dhidi ya walanguzi wa biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu .
Hii leo, msemaji wa polisi ameliambia shirika la habari la dpa kwamba hati nne za kuwezesha kuwakamata kwa walanguzi hao tayari zimeshatolewa na msako kufanywa katika jumla ya nyumba 24 katika miji ya Mannheim na karibu na Karlsruhe na Worms.
Soma: Polisi Ujerumani yatoa video ya mtuhumiwa wa mashambulizi ya mrengo mkali wa kushoto
Msemaji huyo wa polisi amesema kundi linalohusika linadaiwa kuwaleta watu kutoka Mashariki ya Kati na eneo la Caucasus hadi Ujerumani na katika baadhi ya matukio , kuwaruhusu kufanya kazi nchini humo bila ya kuwa na vibali rasmi vya makazi.
Kundi la watu saba wanaodaiwa kufanya biashara hiyo haramu linachunguzwa.
Polisi imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya matukio hayo tangu Januari kwa tuhuma za watu kusafirisha, kuajiri wahamiaji bila vibali vya makazi na udanganyifu.