MigogoroJamhuri ya Kongo
Polisi waliochukua nafasi ya Monusco wakabiliwa na ugumu
2 Mei 2024Matangazo
Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo katika eneo hilo ni pamoja na ukosefu wa mahitaji ya msingi ikiwemo chakula, maji na umeme.
Miongoni mwa vituo vya Umoja wa Mataifa vilivyokabidhiwa kwa mamlaka ya DRC, ni kituo cha Kamanyola katika bonde la Ruzizi.
Soma pia:MONUSCO yasitisha oparesheni zake jimbo la Kivu, Kongo
Ujumbe wa MONUSCO ulithibitisha Jumanne jioni kuwa "operesheni" zake katika jimbo hilo zimefikia tamati, kulingana na matakwa ya serikali ya Kinshasa ambayo ilisema kuwa vikosi hivyo vimeshindwa kabisa kurejesha usalama na utulivu Mashariki mwa Kongo.