Polisi Georgia yawakabili waandamanaji wanaoiunga mkono EU
29 Novemba 2024Matangazo
Polisi katika mji mkuu wa Georgia Tbilisi, wamekabiliana na waandamanaji usiku wa kuamkia leo, baada ya chama tawala cha Georgian Dream, kutangaza kusitisha mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya na kukataa msaada wa bajeti hadi mwaka 2028.
Soma piaBunge la Umoja wa Ulaya latoa wito wa uchaguzi mpya Georgia:
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo ilisema maafisa watatu wa polisi walijeruhiwa. Polisi walitumia maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuvunja lango la bunge.
Mahusiano kati ya Georgia na Umoja wa Ulaya yamezorota hivi karibuni, huku viongozi wa serikali wakiulaumu Umoja wa Ulaya kwa madai ya kujaribu kuchochea mapinduzi nchini humo.