1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland yaongeza shinikizo la kutuma vifaru Ukraine

23 Januari 2023

Poland imesema Jumatatu kuwa itaomba ruhusa ya Ujerumani ili kupeleka nchini Ukraine vifaru chapa Leopard vinavyotengenezwa na Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4Mb6X
Polen Challenger 2 Panzer
Picha: Tomasz Waszczuk/PAP/epa/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Poland, Mateusz Morawiecki hata hivyo amesema kuwa wamejiandaa kuvipeleka hata bila ya idhini ya Ujerumani wakati Ukraine ikiwashinikiza washirika wake kuipelekea zana nzito.

Baada ya siku kadhaa za ongezeko la shinikizo na mkwamo, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Ujerumani haitaiwekea pingamizi Poland ikiwa inataka kupeleka vifaru vya kivita chapa ya Leopard nchini Ukraine.

Poland tayari ilitangaza mapema mwezi huu wa Januari kuwa iko tayari kupeleka vifaru 14 chapa ya Leopard nchini Ukraine, lakini ilikuwa inasubiri taarifa ya wazi kutoka Ujerumani ili kuidhinisha usafirishaji huo. Ujerumani inasisitiza kuhusu haja ya washirika wote kufanya kazi pamoja.