Poland yaishtumu Ujerumani kwa kuingilia mambo yake ya ndani
25 Septemba 2023Rau ametoa wito kwa kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kuheshimu uhuru wa Poland na kumtaka ajiepushe na kauli zinazoharibu mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Chama tawala chakabiliwa na shinikizo kuhusu madai ya kashfa
Chama tawala cha mrengo wa kulia nchini Poland, kinachojinadi kuwa cha "Sheria na Haki", kinakabiliwa na shinikizo kubwa kuhusu madai ya kashfa hizo kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 15 ambapo chama hicho kinawania pia muhula wa tatu madarakani.
Soma pia:EU, Ujerumani zaitaka Poland kujieleza kuhusu rushwa ya visa
Wiki iliyopita, vyombo vya habari vya Poland viliripoti kuwepo kwa mfumo wa rushwa unaoendeshwa na balozi za Poland kwa watu kutoka barani Afrika na Mashariki ya Kati wanaohitaji kuingia katika eneo la mipaka huru linajumuisha mataifa 26 ya Ulaya.
--