1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland kuandaa kura ya maoni kuhusu sera ya uhamiaji Ulaya

13 Agosti 2023

Chama tawala Poland kinataka kuuliza umma katika kura ya maoni kama wanaunga mkono kukaribishwa nchini humo kwa maelfu ya wahamiaji haramu kutoka Mashariki ya Kati na Afrika

https://p.dw.com/p/4V70j
Polen Warschau | 79. Jahrestag des Warschauer Aufstands | Ministerpräsident Mateusz Morawiecki
Picha: Pawel Supernak/PAP/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki ametangaza swali litakaloulizwa katika kura hiyo ya maoni kupitia video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Soma pia: Wahamiaji wanaotafuta ajira waongezeka Ulaya Mashariki

Limeonyesha kuwa chama chake cha Sheria na Haki, kinataka kutumia uhamiaji katika kampeni yake ya uchaguzi mkuu, mbinu ambayo ilikisaidia kuchukua madaraka mwaka wa 2015.

Serikali awali ilisema inataka kuandaa kura ya maoni pamoja na uchaguzi wa bunge unaopangwa Oktoba 15. Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya waliidhinisha mwezi Juni mpango wa kugawana jukumu la kuwahifadhi wahamiaji wanaoingia Ulaya bila vibali, suala ambalo ndio mzizi wa mojawapo ya mizozo ya kisiasa iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya jumuiya hiyo.