1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PLO Lumumba akabiliwa na changamoto katika vita dhidi ya rushwa Kenya

Josephat Nyiro Charo27 Julai 2010

Jinamizi la kashfa ya Angola Leasing ndilo litakalokuwa changamoto ya kwanza itakayomkabili dokta Lumumba

https://p.dw.com/p/OVZY

Mkurugenzi mpya, wa tume ya kupambana na rushwa nchini Kenya Dokta Patrick Lumumba anakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuiendesha tume hiyo.

Hayo yameelezwa na Profesa Tom Namwamba mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka katika chuo kikuu cha Kenyatta mjini Nairobi, Kenya, ambaye ametaja vizingiti kadhaa vinavyomkabili Dokta Lumumba ambaye alianza kazi yake mpya rasmi hapo jana ikiwa ni siku chache tu baada ya shirika la kimataifa la kupambana na rushwa, Transparency International, kutoa ripoti kuhusu rushwa Afrika mashariki, ambapo Kenya inashika nafasi ya tatu baada ya Burundi na Uganda.

Halima Nyanza amezungumza na profesa Namwamba ambaye anataja changamoto hizo.

Mwandishi: Halima Nyanza

Mhariri:Josephat Charo