Katika makala ya Mwangaza wa Ulaya kinachoangaziwa ni hila inayoshuhudiwa barani Ulaya miongoni mwa maafisa wa serikali, mashirika makubwa na watu wenye ushawishi, kutumia mkakati wa mashtaka mahakamani kama njia ya kuwaziba mdomo waandishi habari, watetezi wa mazingira na pia asasi za kiraia, pale wanaharakati hao wanapothubutu kuyapiga kurunzi matendo yao, hususan yale yanayokera kwenye jamii.