1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Paul Kagame kuapishwa leo baada ya ushindi wa kishindo

11 Agosti 2024

Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajiwa kuapishwa leo baada ya kuchaguliwa tena kwa kupata asilimia 99.18 ya kura kwenye uchaguzi uliofanyika Julai 15 na kuongeza muda wake madarakani kwa karibu robo karne.

https://p.dw.com/p/4jLcs
Präsident von Ruanda, Paul Kagame, gibt seine Stimme bei den Präsidentschaftswahlen ab
Rais wa Rwanda Paul Kagame akipiga kura katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatatu, Julai. 15, 2024.Picha: Brian Inganga/AP/picture alliance

Sherehe ya kuapishwa kwake itafanyika katika uwanja wa kitaifa wa Amahoro mjini Kigali.

Maelfu ya Wanyarwanda wakiwemo viongozi wa serikali, mashirika ya kiraia na raia wa kawaida, wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 66.

Soma pia: Changamoto zinazoukabili muhula mpya wa Kagame

Ofisi ya msemaji wa serikali ya Rwanda imetoa taarifa ikieleza kuwa, viongozi kadhaa barani Afrika wanatarajiwa pia kuhudhuria hafla hiyo.

Viongozi ambao tayari wameripotiwa kufika mjini Kigali ni pamoja na Rais William Ruto wa Kenya, Rais Emmerson Mnagangwa wa Zimbabwe, Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini, Umaro Sissoco Embaló wa Guinea-Bissau, Nana Akufo-Addo wa Ghana, miongoni mwa wengine.