1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris:Maurice Papon, mshirika wa Wanazi katika Ufaransa, afariki dunia.

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRA

Mfaransa aliyeshirikiana na watawala wa Kinazi, Maurice Papon, amefarikia dunia akiwa na umri wa miaka 96. Jambo hilo limeelezwa na wakili wake. Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Papon, akiwa Ufaransa, ambayo wakati huo ilitekwa na Wajerumani, alitia saini amri ya kukamatwa na kuhamishwa Wayahudi kutoka nchi hiyo. Baada ya vita alikuwa mkuu wa polisi mjini Paris na baadae waziri wa bajeti. Mwaka 1998, Papon alihukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani. Kutokana na hali yake mbaya ya afya, aitumikia chini ya miaka minne ya kifungo hicho.