Papa Francis awataka makadinali kuweka kando siasa
4 Oktoba 2023Papa Francis ametoa matamshi hayo mbele ya zaidi ya waumini 25,000 iliyotangulia kabla ya kufunguliwa kwa Baraza la viongozi wakuu wa kanisa mjini Vatican linalofahamika kama sinodi.
Baba Mtakatifu Francis amesema siyo jukumu la kanisa kuweka vizuizi kwa kuzingatia mitizamo ya kisiasa na kilimwengu na badala yake lifungue milango watu wote duniani.
"Hatuko hapa kwa mkutano wa bunge au kuweka mpango wa mageuzi. Kongamano la Sinodi siyo bunge, mhusika mkuu hapa ni roho mtakatifu. Hatuko hapa kuunda baraza la kutnga sheria. Tuko hapa kutembea pamoja tukifuata nyayo za Yesu Kristo"
Kongamano hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne, mwaka litajadili nafasi na mwanamke, mtizamano wa kanisa kuhusu watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na taathira za mabadiliko ya tabianchi kwa jamii masikini.