Papa Francis amteua mwanamke nafasi ya juu Vatican
8 Januari 2025Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amemchagua Simona Brambilla kuwa miongoni mwa viongozi wakuu katika moja ya ofisi kuu kwenye makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican.
Uteuzi huo unamfanya Simona kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa kihistoria na kuashiria hatua kubwa ya Papa Francis ya kuwapa wanawake nafasi za uongozi na kuongoza majukumu muhimu ya kanisa hilo, nafasi ambayo haijawahi kutokea huko nyuma.
Soma: Papa Francis asema wanawake wataruhusiwa kupiga kura kwenye mabaraza ya maaskofu
Uteuzi huo wa kihistoria wa Brambilla umethibitishwa na vyombo vya habari huko Vatican, ambavyo viliandika kichwa cha habari vikisema "Mtawa Simona Brambilla ndiye kiongozi wa kwanza mwanamke hapa Vatican".
Papa Fransis alimchagua Simona siku ya Jumatatu na kutangazwa na vyombo vya habari hii leo.