1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis akamilisha ziara yake ya Panama

28 Januari 2019

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amemaliza ziara ya siku tano nchini Panama baada ya kuongoza misa iliyohudhuriwa na maelfu ya vijana katika mji mkuu wa nchi hiyo Panama City.

https://p.dw.com/p/3CIqi
Panama  Papst Franziskus zu Besuch beim Weltjugendtag
Picha: Reuters/A. Bianchi

Katika mahubiri yake Papa Francis aliwatetea wahamiaji wa nchi za Amerika ya Kati na pia amekiri kwamba kanisa Katoliki limeahtirika na kashfa za ngono. Zainab Aziz na taarifa zaidi.

Kabla ya kuwasili Panama Papa Francis ambaye ni Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kati alitoa wito wa kuleta suluhisho la haki na la amani la mgogoro wa nchini Venezuela na pia ametoa wito wa kuleta amani katika nchi jirani ya Colombia iliyokumbwa na chuki za kigaidi.

Baba Mtakatifu amesema baada ya kuhudhuria siku ya vijana duniani, kwamba watu wa Venezuela  wanakabiliwa na hali ngumu lakini amesema sala zake zitaleta matokeo ya kuheshimiwa haki za binadamu.

Kiongozi huo wa kanisa Katoliki duniani amejaribu kuepuka kuegemea upande wowote katika mgogoro wa nchini Venezuela ingawa kanisa Katoliki nchini Venezuela limekuwa linaukosoa vikali utawala wa rais wa kisoshalisti Nicolas Maduro.

Baba mtakatifu pia aliwakumbuka wanafunzi waliouliwa kutokana na chuki za kigaidi nchini Colombia baada ya waasi wa ELN kufanya shambulio la bomu na kuwaua vijana waliokuwa wanafanya mafunzo ya upolisi  mapema mwezi huu. Papa Francis hakujitokeza wazi kulaani vikali mashambulio ya mabomu kwenye kanisa moja nchini Ufilipino na badala yake alitamka tu kuwa jamii ya wakristo imeingia katika majonzi.

Kushoto: Papa Francis alipokutana na rais wa Panama Juan Carlos Varel
Kushoto: Papa Francis alipokutana na rais wa Panama Juan Carlos VarelaPicha: Reuters/Vatican Media

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani amewataka waumini vijana waliohudhuria sala katika mji wa Panama City kuepuka roho iliyokunjika. Aliwanasihi wakristo vijana kurejea kwenye parishi, jamii na familia na kwa marafiki zao ili kubadilishana nao tajiriba ili nao pia wawe na nguvu na ari kama waliyokuwa nayo wao.

Papa Franci amewashauri vijana kusonga mbele kuunda kanisa lakini siyo asambamba na hili lililpo kwani amewaambia kwa kufanya hivyohawatajiletea furaha kubwa na kufikiria kwa njia hiyo hakutawaletea heshima.

Papa Francis pia amewataka wauimini vijana wa kanisa Katoliki wapatao 600,000 kukataa ushawishi wa  maisha ya mitandao ya kijamii na amewataka washiriki zaidi katika harakati za jamii zao. Aliwaambia vijana hao kwamba maisha hayamo katika mawingu yanayosubiri kunakiliwa na kwamba mitandao ya kijamii siyo njia ya kujenga afya ya kiakili.

Pia alionya juu ya umasikini na hatari za usafirishaji wa mihadarati, na dhidi ya baa la mauaji ya wanawake.  Juu ya mpango wa rais wa Marekani Donald Trump wa kujenga ukuta, kiongozi wa kanisa Katoliki duniani aliwaambia maelfu ya waumini, kwamba siyo jambo la busara kwamwadhibu kila mhamiaji na kumwita kuwa tishio kwa jamii.

Mwandishi:Zainab Aziz/AFPE/AP

Mhariri: Iddi Ssessanga