1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ahimiza wema na upendo

25 Desemba 2019

Ujumbe wa papa kuadhmisha krismas umekuja wakati Kanisa Katoliki likikabiliwa na kashfa na upinzani. Licha ya kuwa hakugusia moja kwa moja matatizo ya karibuni, aliyagusia.

https://p.dw.com/p/3VJ5J
Italien Religion l Weihnachtsmesse - Christmette im Vatikan
Picha: AFP/A. Pizzoli

Papa Francis imeeneza ujumbe wa upendo usiyo na masharti katika ujumbe wake wa mkesha wa Krismas mjini Vatican Jumanne jioni. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani aliongoza misa katika kanisa la Mt. Petero kwa maelf ya watu pamoja na wale waliokuwa wanafuatilia kupitia luninga kubwa nje.

"Krismas inatukumbusha kwamba Mungu anaendelea kutupenda sote, hata wale wabaya zaidi miongoni mwetu," alisema Francis katika mahubiri yake.

Papa aliwaambia waumini waliokusanyika mjini Vatican: "Unaweza kuwa na mawazo potofu, unaweza kuwa ulivuruga kila kitu, lakini mungu anaendelea kukupenda. Ni mara ngapi tunafikiri kwamba Mungu ni mwema ikiwa sisi ni wazuri na anatuadhibu ikiwa sisi ni wabaya? Na hivyo ndivyo alivyo."

Nyakati ngumu

Wiki iliyopita Francis alichukuwa hatua nyingine kushughulikia matatizo ya Vatican kwa kufuta sheria ya "usiri wa kipadri", ambayo ndiyo ngazi ya juu zaidi ya usiri katika kanisa katoliki, ambayo haitatumika tena katika kesi za dhulma za kingono dhidi ya mapadri.

Mageuzi hayo yanaondoa kihunzi kikubwa kilichoizuwia polisi kuchunguza uhalifu miongoni mwa mapadri. Vatican pia imekumbwa na wasiwasi kuhusu matumizi mabaya ya kifedha.

Vatikan | Weihnachtsmesse - Christmette im Petersdom
Papa Francis akiongoza misa ya mkesha wa Krismas katika kanisa la Mt. Petero mjini Vatican, Desemba 24, 2019.Picha: Getty Images/AFP/A. Pizzoli

Papa huyo wa 266 aliendelea na mahubiri yake kwa kusema: "Tumtafakari mtoto na tujiache tuingie katika mapendo yake. Kisha hatutakuwa tena na visingizio vya kujiachia kutopendwa na yeye."

Huku kwaya ikiimba wimbo wa "Noel ya kwanza," Francis alielekea chini kwenye jukwaa la kati mwa Kanisa na kuzindua sanamu ya Yesu mchanga aliezaliwa akiwa amelala kwenye madhabau.

Ujumbe wa Krismas

"Chochote kilichokwenda kombo katika maisha yetu," aliendelea. " Chochote kisichokwenda vyema Kanisani, matatizo yoyote tunayokumbana nayo duniani, havitatumika tena kama kisingizio."

Kwenye siku ya Krismas, Francis atatoa hotuba yake inayotolewa mara mbili kwa mwaka ya "Urbe et Orbi" kutokea kwenye roshani ya Kanisa la Mt. Petero kwa makundi ya waumini katika uwanja wa Kanisa.

Tofauti na mahuburi ya mkesha wa Krismas, ujumbe wake siku inayofuata unagusia zaidi umuhimu wa Krismas katika wakati wa mizozo ya jamii ya sasa.

Kwa Francis, aliechaguliwa mwaka 2013, huu ulikuwa mkesha wake wa saba wa Krismas kama Papa. Kabla ya kufungua misa hiyo, Francis aliondoa kipande cha nguo kilichokuwa kimefunika sanamu ya mtoto Yesu, na watoto 12 kutoka Italia, Japan, Venezuela, Kenya, Uganda, Ufilipino na Iraq, waliweka mauawa kwenye madhabahu.