JamiiTimor Mashariki
Papa aitaka Timor Mashariki kuepusha unyanyasaji wa watoto
9 Septemba 2024Matangazo
Timor Mashariki yenye Wakatoliki wengi imekumbwa na mikasa ya watoto kudhulumiwa kingono inayowahusisha pia makasisi ikiwa pamoja na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Askofu Carlos Ximenes, anayedaiwa kuwanyanyasa kingono, watoto wadogo kwa miongo kadhaa.
Papa Francis aliwasili leo nchini Timor Mashariki ikiwa ni nchi ya tatu katika ziara yake ya siku 12 kwenye eneo la Asia-Pasifiki.
Katika ziara hiyo ameshazitembelea Indonesia na Papua New Guinea na atamalizia safari hiyo ndefu kwa ziara ya nchini Singapore.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amesema watu wote wanao wajibu wa kufanya kila linalowezekana ili kuzuia kila aina ya dhulma na kuhakikisha maisha ya utulivu ya utotoni kwa vijana wote.