1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa ato wito wa kusitisha vurugu Mashariki mwa Kongo

16 Juni 2024

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ametoa wito wa kumalizika mapigano na vifo vya raia katika mkoa wa Kivu Kaskazini unaokumbwa na vita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

https://p.dw.com/p/4h6jP
Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa FrancisPicha: Stefano Spaziani/picture alliance

Akizungumza katika uwanja wa St Peters mjini Roma, Papa amesema habari za kuumiza zinazidi kujitokeza za mashambulizi na mauaji Mashariki mwa Kongo. 

Papa ametoa wito kwa serikali na Jumuiya ya Kimataifa kulinda maisha ya raia wa taifa hilo la Afrika. 

Watu 42 wauawa katika shambulizi la waasi wa ADF Kongo

Watu wasiopungua saba waliuwawa siku ya Ijumaa na Jumamosi baada ya watu kuandamana kupinga misururu ya mashambulizi yanayofanywa na waasi wa eneo hilo. 

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki pia amerejelea miito yake ya uwepo wa amani nchini Ukraine, Israel na maeneo ya Palestina, Sudan, Myanmar na maeneo mengine duniani ambako watu wanateseka kwaajili ya vita.