1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMarekani

Papa asikitishwa na mauaji ya New Orleans

2 Januari 2025

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ametoa salamu zake za rambirambi kwa Askofu Mkuu wa New Orleans, Gregory Aymond, kufuatia shambulizi lililotokea katika mji huo wa Marekani, lililowaua watu 15.

https://p.dw.com/p/4olH8
Marekani | Ugaidi | New Orleans
Maafisa wa polisi wamesimama karibu na eneo ambalo gari lilivurumishwa kwenye umati wa watu mjini New Orleans, Marekani.Picha: George Walker IV/AP/picture alliance

Katika barua iliyotumwa kwake na kadinali wa Vatican anayeshughulikia masuala ya mambo ya nje, Pietro Parolin, Papa amesema amesikitishwa sana kusikia taarifa za mauaji na majeruhi yaliyosababishwa na shambulizi hilo.

Amesema Papa anaombea uponyaji kwa waliojeruhiwa na utulivu wa moyo kwa waliofikwa na msiba.

Soma pia: Viongozi wa dunia walaani shambulio la New Orleans, Marekani

Watu 15 waliuwawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa baada ya mwanamume mmoja raia wa Marekani aliye na miaka 42 kutoka Texas, Shamsud-Din Jabbar aliyewahi kuhudumu katika jeshi la taifa hilo kuendesha lori kwenye umati wa watu hapo jana waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya mjini New Orleans.