1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Pande hasimu zimefanya uhalifu wa kivita Sudan

4 Agosti 2023

Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International limesema pande hasimu zinazopambana nchini Sudan zimefanya uhalifu wa kivita katika mgogoro unaondelea.

https://p.dw.com/p/4UmJ1
Sudan West Darfur | Geneina
Picha: Str/AFP

 Ikiwa ni pamoja na mauaji ya makusudi dhidi ya raia na unyanyasaji wa kingono.

Katika ripoti yenye kurasa 56, shirika hilo linabaini kuwa raia waSudan wanauawa na kujeruhiwa kwa kulengwa na mashambulizi, huku wanawake wakibakwa na kuzuiliwa katika mazingira yanayolingana na utumwa wa ngono hasa katika mji mkuu Khartoum na eneo la magharibi la Darfur.

Soma pia:Amnesty Inernational: Pande zinazozozana Sudan zatenda uhalifu wa kivita

Wakijibu ripoti hiyo, jeshilimebaini kuanzisha kitengo maalum cha kujaribu kupunguza madhara kwa raia huku RSF ikikanusha madai hayo.

Sudan ilitumbukia katika machafuko katikati ya mwezi Aprili kufuatia mvutano wa miezi kadhaa kati ya jeshi linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na kundi la RSF la Mohammed Hamdan Daglo.

Mzozo huo tayari umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.