1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pande hasimu za Palestina zakutana Misri kutafuta suluhu

30 Julai 2023

Makundi ya wa Palestina yanayohasimiana yamekutana hii leo nchini Misri kuangazia juhudi za upatanisho wakati vurugu katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa zikiongezeka kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina.

https://p.dw.com/p/4UZ0u
Präsident Mahmoud Abbas
Rais wa Palestina Mahmoud AbbasPicha: MOHAMAD TOROKMAN/REUTERS

Makundi mawili makubwa ya Hamas na Fatah yamegawika tangu mwaka 2007, na majaribio ya kila mara ya kuwapatanisha yameshindwa na hata sasa kukiwa na matarajio hafifu.

Soma zaidi: Hamas yasema bado mapambano yanaendelea Gaza

Kulingana na shirika rasmi la habari la Palestina, Wafa, mazungumzo hayo ya Misri, katika mji wa el-Alamein yataangazia namna ya kurejesha umoja wa kitaifa na kuumaliza mgawanyiko.

Mkutano huo unafanyika wakati machafuko yakiongezeka katika eneo la Ukingo wa Magharibi, ambako rais wa Palestina, mahmoud Abbas na kundi lake la Fatah wamejikita.