Palestina imekuwa mwanachama kamili wa UNESCO
1 Novemba 2011Matangazo
Hatua hiyo iliungwa mkono na theluthi mbili ya wanachama wa shirika hilo la elimu na utamaduni la umoja wa mataifa. Hata hivyo ilikosolewa vikali na Israel na mshirika wake wa karibu Marekani. Ikulu ya Marekani ilisema hatua hiyo inadhohofisha mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Israel na Palestina. Na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Marekani Victoria Nuland amesema Marekani inatarajia kusitisha mchango wake kwa shirika hilo unaonzia kiasi cha dola milioni 60 kwa mwezi huu. Rais wa Palestina aliomba nafasi ya kuwa mwanachama kamili wa UNESCO Septemba mwaka huu.