1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan kuwasaka wakimbizi wasiokuwa na vibali

31 Oktoba 2023

Serikali ya Pakistan imetangaza kuwa itaanza kuwatia nguvuni na kuwashitaki wahamiaji wote wasiokuwa na vibali baada ya muda wa mwisho iliowapa kumalizika, hatua inayoonekana kuwalenga zaidi wakimbizi kutoka Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4YFGr
Wakimbizi wa Afghanistan nchini Pakistan wakingojea utaratibu wa idara ya uhamiaji kwenye mpaka wa jimbo la Peshawar.
Wakimbizi wa Afghanistan nchini Pakistan wakingojea utaratibu wa idara ya uhamiaji kwenye mpaka wa jimbo la Peshawar.Picha: Hussain Ali/ZUMA Wire/IMAGO

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan, Sarfraz Bugti, alisema siku ya Jumanne (Oktoba 31) katika taarifa ya video iliyorekodiwa kuwa "zimebaki siku mbili tu kwa wahamiaji hao kurudi nyumbani kwao kwa hiari."

"Muda wa mwisho uliowekwa wa Novemba Mosi utamalizika kesho Jumatano."Aliongeza.

Soma zaidi: Wakimbizi 10,000 wa Afghanistan wakimbilia mpaka wa Pakistan

Waziri huyo wa serikali ya mputo alisema baada ya hapo operesheni yao ndefu na ya taratibu itaanza kwa kuhakikisha kuwa hawawafukuzi wakimbizi wowote.

Pakistan ina wahamiaji na wakimbizi zaidi ya milioni nne wa Kiafghanistani na karibu milioni 1.7 kati yao hawana vibali maalumu, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani.

Idadi hiyo ni pamoja na wengi waliozaliwa Pakistan na ambao wameishi huko maisha yao yote.

Tayari zaidi ya Waafghanistani 10,000 wanaoishi Pakistan walikuwa wameshakimbilia mipakani siku ya Jumanne, wakihofia kukamatwa.