SiasaPakistan
Pakistan yaihimiza Iran kushirikiana kiusalama
19 Januari 2024Matangazo
Wito huo ameutoa leo katika mazungumzo yake ya simu na waziri mwenzake wa Iran, ambapo ameelezea utayari wa Pakistan kushirikiana na Iran katika masuala yote.
Viongozi hao wa mataifa jirani wamezungumza siku moja baada ya Pakistan kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika kile ilichosema yaliyalenga maeneo ya wanamgambo nchini Iran, kutokana na Iran kufanya mashambulizi wiki hii kuzilenga ngome za wanamgambo nchini Pakistan.
Mazungumzo hayo ya simu yamefanyika baada ya Pakistan kusema haitaki kuzidisha mzozo kati yake na Iran. Hayo yamebainika katika mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu wa kiraia na kijeshi uliofanyika leo kutathmini hali ya usalama baada ya nchi hizo mbili kushambuliana kwa makombora.