SiasaUswidi
OIC yatoa wito wa hatua dhidi ya visa vya kuinajis Quran
2 Julai 2023Matangazo
Kauli hiyo iliyoripotiwa na televisheni ya taifa ya Saudi Arabia imetolewa wakati wa mkutano wa dharura ulioitishwa baada ya mwanaume mmoja kuchana na kuchoma Koran nchini Sweden wiki iliyopita.
Katika tukio hilo mwanaume huyo aliyejitambulisha kuwa mkimbizi kutoka Iraq alifunguliwa mashtaka. Licha ya kuwa polisi nchini Sweden imekuwa ikikataa maombi kadhaa ya mandamano ya hivi karibuni, mahakama nchini humo zimekuwa zikitupilia mbali maamuzi hayo kwa madai kuwa yanakiuka haki ya uhuru wa kujieleza.