1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyota wa mpira wa kikapu Dikembe Mutombo aaga dunia

Josephat Charo
1 Oktoba 2024

Nyota wa mpira wa kikapu raia wa Congo na Marekani Dikembe Mutombo ameaga dunia baada ya kuugua saratani ya ubongo.

https://p.dw.com/p/4lGWO
Nyota wa mpira wa kikapu raia wa Congo na Marekani, Dikembe Mutombo
Nyota wa mpira wa kikapu raia wa Congo na Marekani, Dikembe MutomboPicha: Shannon Finney/Getty Images

Nyota wa mchezo wa kikapu raia wa Congo na Marekani Dikembe Mutombo, aliyefahamika sana kama mojawapo ya wachezji wazuri kabisa wa ulinzi katika hisotria ya ligi ya mchezo wa kikapu nchini Marekani NBA, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58. 

Mutombo aliaga dunia akiwa amezungukwa na familia yake baada ya kuugua saratani ya ubongo. Kamishna wa NBA Adam Silber amesema uwanjani Dikembe Mutombo alikuwa miongoni mwa walinzi bora aliyezuia mipira katika historia ya NBA na nje ya uwanja alikuwa na moyo wa kuwasaidia watu wengine.

Mutombo, ambaye alicheza kwa misimu 18 katika ligi ya NBA alifanya juhudi kubwa kuboresha hali ya maisha katika nchi yake alikozaliwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia wakfu wake binafsi.

Dikembe Mutombo alistaafu NBA mnamo 2009 baada ya kuchezea timu kadhaa zikiwamo Denver Nuggets, Atlanta Hawks, Philadelphia, New Jersey Nets, New York Knicks na Houston Rockets.