Biashara
Makampuni ya Ujerumani yakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi
29 Novemba 2023Matangazo
Ujerumani, kama tu ilivyo katika nchi nyingine zilizostawi kiviwanda kote duniani, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi, hasa katika sekta za ujuzi wa ukuaji wa juu.
Soma pia: Ujerumani kuwa nchi ya pekee barani Ulaya kuingia kwenye mdororo wa uchumi 2023
Achim Dercks, Naibu Afisa Mkuu Mtendaji wa DHIK amesema hali ya upatikanaji wa wafanyakazi wenye ujuzi bado ni mbaya sana. Kwa mujibu wa makadirio ya karibuni, nafasi za ajira milioni 1.8 hazijajazwa katika uchumi wa Ujerumani kwa ujumla.
Dercks anasema hiyo inamaanisha zaidi ya euro bilioni 90 katika thamani ya ziada zitapotea mwaka huu. Hii ni sawa na zaidi ya asilimia mbili ya pato jumla la nchi.