SiasaLebanon
Norway na Uswisi zataka uchunguzi huru wa mripuko Beirut
10 Februari 2023Matangazo
Mataifa wanachama katika Umoja wa Ulaya, Norway na Uswisi yamewataka wadau muhimu nchini Lebabnon kutoa nafasi ya uchunguzi huru na wa haki kuhusu mripuko wa bandari ya Beirut. Na kujiweka kando na uingiliaji wowote.
Taarifa hiyo imetoa wito kwa bunge kushiriki dharura ya kumchagua rais ambae atawaunganisha raia wa Lebanon kwa maslahi ya taifa ikiwa ni hatoa ya mwanzo kurejesha taasisi za taifa hilo katika kufanya maamuzi kiutawala na kisiasa.
Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na balozi za Uswisi na Norway zimeonyesha hali ya wasiwasi mkubwa katika taarifa hiyo ya pamoja kuhusu hali ya sasa nchini Lebanon.