1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Njia za kupunguza uzito

25 Julai 2012

Binadamu tumeumbwa kwa namna tofauti - weupe, weusi, warefu na wafupi, wembamba na wanene - na wapo walioridhika na maumbile na maumbo yao huku wengine wakifanya kila liwezekanalo kuubadili mtazamo wao wa nje.

https://p.dw.com/p/15dnr
Upunguzaji wa uzito.
Upunguzaji wa uzito.Picha: Fotolia/Gorilla

Wakati katika nchi za Magharibi wengi wanapendelea kuwa na miili myembamba, katika nchi nyingi za Kiafrika, unene unaonekana kama ishara ya utajiri. Hata hivyo wapo watu wanaopenda kupunguza uzito, iwe kwa sababu za kiafya au za kimwonekano. Katika makala hii ya Afya Yako, Elizabeth Shoo anazungumzia njia mbali mbali za kupunguza uzito, faida na athari zake, msisitizo ukiwa ni mtu kujijali na kujikubali. Kusikiliza makala hii, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Elizabeth Shoo
Mhariri: Josephat Charo